Mkuu wa Chuo Cha Habari Maalum kushoto na Mwalimu Christopher Sign, | Picha na Grace Lawi. |
Saturday, February 27, 2016
Picha ya pamoja baada ya kumaliza Course ya Writing for Media na mwalimu Christopher Sign.
Umoja wa wanafunzi wa chuo cha Habari Maalum watembelea kituo cha watoto yatima Yeriko kilichopo Ngaramtoni Arusha.
Umoja
wa wanafunzi wa chuo cha Habari Maalum watembelea kituo cha watoto yatima
Yeriko kilichopo Ngaramtoni Arusha.
Na Grace Lawi,
Wanafunzi wa chuo cha Habari Maalum wamewatembelea
watoto yatima katika moja ya vituo vya watoto yatima.
Hayo yamesemwa na Rais wa chuo Bwn, Wilfred
Mikomangwa alipokuwa akiwashukuru wanafunzi hao kwakuonyesha juhudi zao katika
swala hilo, wakati wa ibada fupi ya jioni chuoni hapo.
Wanafunzi hao wameonyesha muhamko mkubwa sana juu ya
swala hili kwani kila ifikapo mwisho wa mwezi kiwango cha utoaji kinaungezeka
maradufu.
Aidha, waalimu wachuo hicho hawapo nyuma kuonyesha
ushirikiano wao na wanafunzi katika kufanikisha swala hilo.
Hata hivyo, Serekari ya wanafunzi katika chuo hicho, wamekuwa bega kwa bega na wanafunzi hao na kuonyesha mfano mzuri, katika kuchangia pia na kwenda kuwatembelea watoto hao.
News
ZIARA
YA SEREKALI KATIKA CHUO CHA HABARI
MAALUM ARUSHA
Na
Grace lawi,
Uongozi wa chuo cha Habari Maalum umepongezwa
kwaufanisi na jitihada katika kuboresha taaluma kwa nadharia na vitendo katika vitengo
vyake.
Hayo yamesemwana Mkuu wa wilaya ya Arumeru,
Bwana Elisha Nkhambaku, alipotembelea chuo hicho nakuzungumza na uongozi wa chuo kuhusu
maendeleo ya taaluma chuoni hapo.
Naye Mkuu wa chuo hicho bwana Jackson
Kaluzi, amebainisha mafanikio yaliyofikiwa kuwa nipamoja na wanafunzi
waliohitimu mwaka jana baadhi yao kupata kazi katika
kituo cha habari cha star tv kilichopo mkoani Mwaza baada ya kufanya vizuri katika
mazoezi kwa vitendo.
Aidha, Bwana Kaluzi ameelezea changamoto
kubwa chuoni hapo kuwa nipamoja na uhaba wa wanafunzi kwani chuo hicho kina uwezo
wakuchukua wanafunzi zaidi ya mia mbili.
Sanjarinahayo, Bwana Nkhambaku, ameahidi
kuwabega kwa bega na chuo kwa kutangaza chuo hicho ili kupata wanafunzi wengi zaidi
katika vitengo vya habari na mawasiliano pamoja na uongozi na utawala.
Subscribe to:
Posts (Atom)