ZIARA
YA SEREKALI KATIKA CHUO CHA HABARI
MAALUM ARUSHA
Na
Grace lawi,
Uongozi wa chuo cha Habari Maalum umepongezwa
kwaufanisi na jitihada katika kuboresha taaluma kwa nadharia na vitendo katika vitengo
vyake.
Hayo yamesemwana Mkuu wa wilaya ya Arumeru,
Bwana Elisha Nkhambaku, alipotembelea chuo hicho nakuzungumza na uongozi wa chuo kuhusu
maendeleo ya taaluma chuoni hapo.
Naye Mkuu wa chuo hicho bwana Jackson
Kaluzi, amebainisha mafanikio yaliyofikiwa kuwa nipamoja na wanafunzi
waliohitimu mwaka jana baadhi yao kupata kazi katika
kituo cha habari cha star tv kilichopo mkoani Mwaza baada ya kufanya vizuri katika
mazoezi kwa vitendo.
Aidha, Bwana Kaluzi ameelezea changamoto
kubwa chuoni hapo kuwa nipamoja na uhaba wa wanafunzi kwani chuo hicho kina uwezo
wakuchukua wanafunzi zaidi ya mia mbili.
Sanjarinahayo, Bwana Nkhambaku, ameahidi
kuwabega kwa bega na chuo kwa kutangaza chuo hicho ili kupata wanafunzi wengi zaidi
katika vitengo vya habari na mawasiliano pamoja na uongozi na utawala.
No comments:
Post a Comment