Wednesday, April 20, 2016

Trump na Clinton washinda New York


Furaha ya ushindi mjini New York

Zaidi ya nusu ya kura zilizohesabiwa katika uchaguzi wa awali wa urais nchini marekani katika mji wa New york,zinaonesha kwamba Donald Trump na Hillary Clinton wamepata ushindi mkubwa Zaidi ndani ya vyama vyote viwili.

Hillary Clinton ambaye amemshinda mpinzani wake Bernie Sanders kwa ushindi mkubwa ameeleza katika hotuba yake kuwa ushindi wa chama chake cha Democratic umeweza kuwaunganisha zaidi wapinzani wake kuwa wamoja Zaidi ya kuwagawa.

Hata hivyo New York inatajwa kuwa ngome nyingine ya Donald Trump,ambapo Cruz yeye hesabu za kura zake zimeonekana kugoma mapema kabisa katika chama chake cha Repubilcan .

Wakati Hillary Clinton amemshinda mpinzani wake Bernie Sanders kwa ushindi mkubwa .Hillary amewaambia wapinzani wake kuwa kuna la ziada linalowafanya wawe wamoja Zaidi ya kuwagawa.

Chanzo BBCswahili.
 

Tuesday, April 19, 2016

Grace lawi Jackson: Mugabe amlalamikia askofu kuhusu ndoa za jinsia mo...

Grace lawi Jackson: Mugabe amlalamikia askofu kuhusu ndoa za jinsia mo...: Rais Mugabe hupinga sana wapenzi wa jinsia moja   Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe alikutana na Askofu mkuu wa Canterbury na kuibua m...

Mugabe amlalamikia askofu kuhusu ndoa za jinsia moja


Rais Mugabe hupinga sana wapenzi wa jinsia moja

 Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe alikutana na Askofu mkuu wa Canterbury na kuibua maswali kuhusu ndoa za wapenzi wa jinsia moja.

Askofu mkuu Justin Welby amesema alimjibu kiongozi huyo kwamba kuna mitazamo tofauti kuhusu ndoa hizo miongoni mwa waumini wa kanisa la Kianglikana kote duniani.

Aliongeza hata hivyo kwamba wengi wa waumini wanaamini ndoa ni uhusiano wa muda mrefu baina ya mwanamume na mwanamke.

Askofu Welby alisema ni makosa kuwahukumu au kuwaadhibu watu kwa sababu ya msimamo wao kijinsia na kimapenzi.

Hata hivyo, amesema dalili zilionesha Bw Mugabe hakukubaliana naye.

“Sidhani itakuwa haki kusema kwamba Bw Mugabe alikubaliana nami kabisa,” alisema Askofu Welby.

Mkutano huo wa faraghani ulifanyika mjini Harare, baada ya Askofu Welby, ambaye yumo katika taifa jirani la Zambia anakohudhuria mkutano wa viongozi wa kanisa la Kiangilikana kufanya ziara fupi Zimbabwe.

Msemaji wa Lambeth Palace amesema mpango huo ulipangwa dakika za mwishomwisho na ulidumu chini ya saa moja.

Bw Mugabe ni Mkatoliki na hupinga sana ndoa za wapenzi wa jinsia moja.
Askofu Welby amesema Bw Mugabe hakukubaliana naye kabisa
Maafisa wa kanisa hilo wamesema mkutano huo ulikuwa sana wa kidini badala ya kisiasa ingawa uhusiano baina ya serikali na kanisa ulijadiliwa.

Chanzo BBCswahili

Magufuli ataka daraja lipewe jina la Nyerere

Daraja la kigamboni lina urefu wa mira 680
Rais wa Tanzania John Magufuli amependekeza daraja mpya la Kigamboni lipewe jina la mwanzilishi wa taifa hilo Mwalimu Julius Nyerere.

Akiongea muda mfupi kabla ya kuzindua rasmi daraja linafaa kupewa jina la Mwalimu Julius Nyerere kutokana na mchango wake kwa nchi hiyo.

Daraja la Kigamboni lilianza kutumika tarehe 16 Aprili, 2016 na lina urefu wa mita 680 na barabara unganishi upande wa Kurasini na Kigamboni zenye urefu wa kilomita 2.5.
Rais Magufuli baada ya kuzindua daraja la Kigamboni
 Ujenzi wake ulifanywa na kampuni ya China Railway 15 Group ikishirikiana na kampuni ya China Bridge Engineering Group.

Daraja hilo ndilo la kwanza la kubeba uzito wa barabara kwa kutumia nyaya Afrika Mashariki na la tatu Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara bila kuhesabu Afrika Kusini.

Linamilikiwa na serikali ya Tanzania na Hazina ya Malipo ya Uzeeni (NSSF) kwa 40% na 60% mtawalia na litachukua nafasi ya feri ya MV Magogoni.
Wenye magari watalipia kutumia barabara hiyo
 Wenye magari na pikipiki watahitajika kulipa kutumia daraja hilo lakini wapitanjia watavuka bila malipo.

Ujenzi wa daraja hilo, ambao uligharimu dola 128 milioni za Kimarekani, ulianza mwaka 2012.

Chanzo BBCswahili.