![]() |
Daraja la kigamboni lina urefu wa mira 680 |
Rais wa Tanzania John Magufuli
amependekeza daraja mpya la Kigamboni lipewe jina la mwanzilishi wa taifa hilo
Mwalimu Julius Nyerere.
Akiongea muda mfupi kabla ya
kuzindua rasmi daraja linafaa kupewa jina la Mwalimu Julius Nyerere kutokana na
mchango wake kwa nchi hiyo.
Daraja la Kigamboni lilianza
kutumika tarehe 16 Aprili, 2016 na lina urefu wa mita 680 na barabara unganishi
upande wa Kurasini na Kigamboni zenye urefu wa kilomita 2.5.
![]() |
Rais Magufuli baada ya kuzindua daraja la Kigamboni |
Ujenzi wake ulifanywa na kampuni ya
China Railway 15 Group ikishirikiana na kampuni ya China Bridge Engineering
Group.
Daraja hilo ndilo la kwanza la
kubeba uzito wa barabara kwa kutumia nyaya Afrika Mashariki na la tatu Afrika
kusini mwa Jangwa la Sahara bila kuhesabu Afrika Kusini.
Linamilikiwa na serikali ya Tanzania
na Hazina ya Malipo ya Uzeeni (NSSF) kwa 40% na 60% mtawalia na litachukua
nafasi ya feri ya MV Magogoni.
![]() |
Wenye magari watalipia kutumia barabara hiyo |
Wenye magari na pikipiki
watahitajika kulipa kutumia daraja hilo lakini wapitanjia watavuka bila malipo.
Ujenzi wa daraja hilo, ambao
uligharimu dola 128 milioni za Kimarekani, ulianza mwaka 2012.
Chanzo BBCswahili.
No comments:
Post a Comment