![]() |
Furaha ya ushindi mjini New York
|
Zaidi ya nusu ya kura zilizohesabiwa
katika uchaguzi wa awali wa urais nchini marekani katika mji wa New
york,zinaonesha kwamba Donald Trump na Hillary Clinton wamepata ushindi mkubwa
Zaidi ndani ya vyama vyote viwili.
Hillary Clinton ambaye amemshinda
mpinzani wake Bernie Sanders kwa ushindi mkubwa ameeleza katika hotuba yake
kuwa ushindi wa chama chake cha Democratic umeweza kuwaunganisha zaidi
wapinzani wake kuwa wamoja Zaidi ya kuwagawa.
Hata hivyo New York inatajwa kuwa
ngome nyingine ya Donald Trump,ambapo Cruz yeye hesabu za kura zake zimeonekana
kugoma mapema kabisa katika chama chake cha Repubilcan .
Wakati Hillary Clinton amemshinda
mpinzani wake Bernie Sanders kwa ushindi mkubwa .Hillary amewaambia wapinzani
wake kuwa kuna la ziada linalowafanya wawe wamoja Zaidi ya kuwagawa.
Chanzo BBCswahili.
No comments:
Post a Comment