Tume ya Umoja wa Afrika imetangaza
kwamba itawatuma waangalizi wa uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar ambao
utafanyika Jumapili.
Mwenyekiti wa tume hiyo Dkt
Nkosazana Dlamini Zuma ameidhinishwa kutumwa kwa wataalamu sita wa kufuatilia
uchaguzi huo wa tarehe 20 Machi.
Vyama sita vya upinzani, kikiwemo
Chama cha Wananchi (CUF) vimetangaza kwamba vitasusia uchaguzi huo.
Uchaguzi huo unatokana na kufutwa
kwa matokeo ya uchaguzi wa urais na wawakilishi uliofanyika tarehe 25 Oktoba
mwaka jana.
Chama cha CUF kilipinga hatua ya kufutwa kwa
matokeo hayo.
Mgombea wake wa urais, Maalim Seif
Sharif Hamad, alijitangaza mshindi wa uchaguzi huo wa mwaka jana
Juhudi za kutumia mazungumzo
kutafutia ufumbuzi mzozo wa kisiasa uliotokana na kufutwa kwa matokeo hayo
hazikufua dafu.
Kupitia taarifa, AU imesema:
“Kuambatana na wajibu wake, Tume ya Umoja wa Ulaya itatuma ujumbe wa wataalamu
Zanzibar kuhakikisha kwamba uchaguzi wa marudio ni wa amani, wa kuaminika na
unatimiza viwango vya AU vya uchaguzi wa kidemokrasia.”
Ujumbe huo utakuwa visiwani Zanzibar
kati ya tarehe 17 na 25 Machi.
Chanzo BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment