![]() |
May amemrithi David Cameron aliyejiuzulu baada ya kura ya maoni |
Waziri mkuu mpya wa
Uingereza Theresa May leo amepangiwa kufanya ziara yake ya kwanza
ng’ambo kama waziri mkuu ambapo ataelekea mjini Berlin, Ujerumani
kukutana na kansela wa Ujerumani Angela Merkel.
Viongozi hao
wawili watajadili utaratibu wa Uingereza kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya
baada ya raia nchini humo kuidhinisha hatua hiyo kwenye kura ya maoni
mwezi uliopita.Kadhalika, watajili uhusiano wa kibiashara wa siku zijazo.
![]() |
Bi Merkel amekuwa na ushawishi mkubwa Ulaya |
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter
Steinmeier, amesema anatarajia Uingereza kuchukua hatua haraka kumaliza
hali ya sintafahamu ambayo imetanda tangu kufanyika kwa kura ya maoni
Uingereza.
Waandishi wa habari wanasema kuanzisha uhusiano wa moja
kwa moja baina yake na Bi Merkel litakuwa jambo muhimu sana kwa Bi May
anapojaribu kufanikisha mazungumzo ya kuwezesha Uingereza kujiondoa
vyema kutoka kwa EU.Chanzo BBC
No comments:
Post a Comment