Thursday, July 21, 2016

Kijana mweusi amefariki mikononi mwa polisi UFARASA


Polisi wakikabiliana na waandamanaji awali mjini Paris
 Na Grace Lawi
 Waandamanaji wameungana kukabiliana na maafisa wa polisi katika mji wa BEAUMONT-SUR-OISE huko UFARASA  baada ya kijana mweusi kufariki akiwa kizuizini.

Mabomu ya petroli yamerushwa na maafisa wa polisi na taarifa zinasema waandamanaji walijaribu kuteketeza ukumbi wa mji huku watu wanne wamekamatwa na kuzuiliwa.

Polisi wanasema Adama Traore alipata mshtuko wa moyo Jumanne baada yake kuzuiliwa katika mji huo ulioko kilomita thelathini kaskazini mwa Paris.

Lakini marafiki zake wanasema alikuwa buheri wa afya kabla ya kukamatwa na kwamba alipigwa na maafisa hao wa polisi hata hivyo uchunguzi wa kubaini chanzo cha kifo chake utafanywa baadaye Alhamisi.

Miaka 11 iliyopita, vifo vya vijana wawili waliokuwa wakijaribu kukwepa kukamatwa vilisababisha maandamano yaliyodumu wiki mbili katika viunga vya mji wa Paris na miji mingine nchini humo.

Tahadhari mpya ya kiusalama yatangazwa nchini UTURUKI



Na Grace Lawi
Maelfu ya wananchi wanaokubaliana na msimamo wa serikali ya UTURUKI wamekusanyika  katika viwanja vya KIZILAY mjini ANKARA kuunga mkono kauli ya RAIS RECEP TAYYIP ERDOGAN kuhusu tahadhari mpya ya kiusalama nchini humo.

Mmoja wa viongozi wanaoiunga mkono serekali amesema wanakubaliana na   msimamo wa RAIS ERDOGAN  na kwamba watafanya lolote atakalosema kwakua yeye ndie mtu wanayemwamini na kumfuata.

Tayari  tahadhari zinaendelea kuchukuliwa kwa washukiwa wakijeshi na waungaji mkono wa mapinduzi katika maeneo mbalimbali nchini humo huku takwimu zikionyesha takribani watu elfu sitini  wamekamatwa au kutiwa hatiani.

Chanjo dhidi ya HIV kufanyiwa majaribio Afrika


       Maendeleo kwenye chanjo ya HIV ndio suala kuu katika mkutano wa dunia wa ukimwi. Mtaalam wa juu wa ukimwi anasema hawezi kusema lini tiba ya HIV na Ukimwi huwenda ikaptiakana, lakini anasema amefurahishwa na maendeleo yake.

    Wanasayansi wanaohudhuria mkutano wa 21 wa kimataifa wa Ukimwi mjini Durban Afrika kusini wanasema bado hakuna chanjo ya kuzuia maambukizo ya HIV na ukimwi.

    Mkurugenzi wa taasisi ya kitaifa ya kimarekani ya afya na magonjwa ya kuambukiza Dr Anthony Fauci, anasema ni vigumu kutabiri pale chanjo dhidi ya HIV na ukimwi itapatikana, lakini anasema anamatumaini kuwa wanakaribia kupata tiba.

    Japo hakuna chanjo maalum ambayo imeonyesha matumaini, lakini wanayasayansi wanaendelea kwa dhati na majaribio ya chanjo HVTN 702.

    Chanjo hio inayofanyiwa majaribio ilitokana na majaribio yalofanywa nchini Thailand miaka michache ilopita na inaonyesha kiwango fulani cha ufanisi.

    Majaribio ya chanjo hiyo yanategemewa kuanza huko Afrika kusini na katika baadhi ya mataifa mengine ya Afrika baadae mwaka huu, lakini Dr. Fauci amesema itachukuwa muda kabla matokeo kupatikana.

Wednesday, July 20, 2016

Donald Trump kugombea urais Marekani


Donald Trump
DONALD TRUMP ameteuliwa rasmi  kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha REPUBLICAN,mara baada ya uungwaji mkono na wajumbe kutoka majimbo na wilaya za Marekani katika kura mchujo iliyofanyika  mjini CLEVELAND.

TRUMP ameuambia mkutano wa kitaifa wa chama cha Rebuplican kwamba anajivunia kuwa mgombea wa chama hicho katika uchaguzi wa urais mwezi Novemba mwaka huu na atashinda kura hiyo ili kuleta mabadiliko halisi kwa Washington.

Naye Spika wa bunge la wawakilishi, PAUL RYAN ameomba wajumbe kwenye kikao hicho kumuunga mkono TRUMP akieleza kuwa kutakuwa na uhakika wa ushindi iwapo tu wanachama wote wa Republican watashirikiana.
Chanzo BBC.

May kukutana na Merkel Ujerumani

May amemrithi David Cameron aliyejiuzulu baada ya kura ya maoni
 Waziri mkuu mpya wa Uingereza Theresa May leo amepangiwa kufanya ziara yake ya kwanza ng’ambo kama waziri mkuu ambapo ataelekea mjini Berlin, Ujerumani kukutana na kansela wa Ujerumani Angela Merkel.
Viongozi hao wawili watajadili utaratibu wa Uingereza kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya baada ya raia nchini humo kuidhinisha hatua hiyo kwenye kura ya maoni mwezi uliopita.
Kadhalika, watajili uhusiano wa kibiashara wa siku zijazo.



Bi Merkel amekuwa na ushawishi mkubwa Ulaya
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier, amesema anatarajia Uingereza kuchukua hatua haraka kumaliza hali ya sintafahamu ambayo imetanda tangu kufanyika kwa kura ya maoni Uingereza.
Waandishi wa habari wanasema kuanzisha uhusiano wa moja kwa moja baina yake na Bi Merkel       litakuwa jambo muhimu sana kwa Bi May anapojaribu kufanikisha mazungumzo ya kuwezesha Uingereza kujiondoa vyema kutoka kwa EU.

Chanzo BBC