![]() |
Maelfu ya wananchi wanaokubaliana na msimamo wa serikali ya UTURUKI wamekusanyika katika viwanja vya KIZILAY mjini ANKARA kuunga mkono kauli ya RAIS RECEP TAYYIP ERDOGAN kuhusu tahadhari mpya ya kiusalama nchini humo.
Mmoja wa viongozi wanaoiunga mkono serekali amesema wanakubaliana na msimamo wa RAIS ERDOGAN na kwamba watafanya lolote atakalosema kwakua yeye ndie mtu wanayemwamini na kumfuata.
Tayari tahadhari zinaendelea kuchukuliwa kwa washukiwa wakijeshi na waungaji mkono wa mapinduzi katika maeneo mbalimbali nchini humo huku takwimu zikionyesha takribani watu elfu sitini wamekamatwa au kutiwa hatiani.
No comments:
Post a Comment