Thursday, July 21, 2016

Kijana mweusi amefariki mikononi mwa polisi UFARASA


Polisi wakikabiliana na waandamanaji awali mjini Paris
 Na Grace Lawi
 Waandamanaji wameungana kukabiliana na maafisa wa polisi katika mji wa BEAUMONT-SUR-OISE huko UFARASA  baada ya kijana mweusi kufariki akiwa kizuizini.

Mabomu ya petroli yamerushwa na maafisa wa polisi na taarifa zinasema waandamanaji walijaribu kuteketeza ukumbi wa mji huku watu wanne wamekamatwa na kuzuiliwa.

Polisi wanasema Adama Traore alipata mshtuko wa moyo Jumanne baada yake kuzuiliwa katika mji huo ulioko kilomita thelathini kaskazini mwa Paris.

Lakini marafiki zake wanasema alikuwa buheri wa afya kabla ya kukamatwa na kwamba alipigwa na maafisa hao wa polisi hata hivyo uchunguzi wa kubaini chanzo cha kifo chake utafanywa baadaye Alhamisi.

Miaka 11 iliyopita, vifo vya vijana wawili waliokuwa wakijaribu kukwepa kukamatwa vilisababisha maandamano yaliyodumu wiki mbili katika viunga vya mji wa Paris na miji mingine nchini humo.

No comments:

Post a Comment