Thursday, March 17, 2016

AU kutuma waangalizi wa uchaguzi Zanzibar



Tume ya Umoja wa Afrika imetangaza kwamba itawatuma waangalizi wa uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar ambao utafanyika Jumapili.

Mwenyekiti wa tume hiyo Dkt Nkosazana Dlamini Zuma ameidhinishwa kutumwa kwa wataalamu sita wa kufuatilia uchaguzi huo wa tarehe 20 Machi. 

Vyama sita vya upinzani, kikiwemo Chama cha Wananchi (CUF) vimetangaza kwamba vitasusia uchaguzi huo.

Uchaguzi huo unatokana na kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais na wawakilishi uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka jana.

Chama cha CUF kilipinga hatua ya kufutwa kwa matokeo hayo.
Mgombea wake wa urais, Maalim Seif Sharif Hamad, alijitangaza mshindi wa uchaguzi huo wa mwaka jana
Juhudi za kutumia mazungumzo kutafutia ufumbuzi mzozo wa kisiasa uliotokana na kufutwa kwa matokeo hayo hazikufua dafu.

Kupitia taarifa, AU imesema: “Kuambatana na wajibu wake, Tume ya Umoja wa Ulaya itatuma ujumbe wa wataalamu Zanzibar kuhakikisha kwamba uchaguzi wa marudio ni wa amani, wa kuaminika na unatimiza viwango vya AU vya uchaguzi wa kidemokrasia.”

Ujumbe huo utakuwa visiwani Zanzibar kati ya tarehe 17 na 25 Machi.

Chanzo BBC Swahili.

Wednesday, March 9, 2016

Kuchati ni marufuku katika wizara




Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania imewapiga marufuku wafanyakazi wake ''Kuchati'' katika mitandao ya kijamii kwa kutumia simu katika muda wa saa za kazi.

Waziri wa Wizara hiyo Makame Mbarawa amekemea tabia ya baadhi ya wafanyakazi, kutumia muda mwingi maofisini kuperuzi katika mitandao ya kijamii pamoja na kupiga porojo, hali inayosababisha kushuka kwa uzalishaji na maendeleo.

Ameongeza kuwa watakaobainika kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria bila ya kuonewa haya, na pia kuwataka wafanyakazi wa wizara yake kuwa na bidii ya kazi na weledi.
 
Watu wengi hutumia simu za mikononi na kompyuta, kwa lengo la kupata taarifa mbalimbali na pia kujifunza. ( Picha na Maktaba )
Lakini hata hivyo, marufuku hiyo itaweza kufanikiwa?, kutokana na ukubwa wa matumizi ya mtandao, huku walengwa wakiona wananufaika nayo.

Kutokana na kukua kwa teknolojia ya habari na mawasiliano duniani, watu wengi hususan vijana wamekuwa wakitumia muda mwingi katika mitandao ya kijamii, kupitia simu za mikononi na kompyuta, kwa lengo la kupata taarifa mbalimbali za ulimwengu na pia kujifunza.

Nchini Tanzania matumizi ya huduma ya mawasiliano imekuwa kwa kasi katika siku za hivi karibuni, hususan kupitia mitandao ya WhatsApp, Facebook, Twitter na blogi mbalimbali.

 Chanzo BBC swahili.

Friday, March 4, 2016

Waziri wa zamani wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa aaga dunia.



Na Grace Lawi,

WAZIRI wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Joseph Rwegasira amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.

Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa imethibitisha kifo hicho kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Rwegasira aliyeiongoza wizara hiyo kati ya mwaka 1993 na 1995, wakati wa utawala wa Serikali ya Awamu ya Pili iliyoongozwa na Rais Ali Hassan Mwinyi, alifikwa na mauti jana.

Msiba upo nyumbani kwa marehemu Msasani, Dar es salaam.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kesho mwili wa Balozi Rwegasira utaagwa katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro, Oysterbay Mbuyuni saa 8.00 mchana na utasafirishwa keshokutwa kwenda Bukoba, Kagera kwaajili ya mazishi.

Chanzo: Habari Leo

WEATHER FORECAST FOR TODAY


Arusha
Temp: 30°C / 19°C
Sun rise: 06:43
Sun set: 18:51
Weather: partly cloudy and light rain
Wind: E at 10km/hr

Kilimanjaro
Temp: 35°C / 23°C
Sun rise: 06:41
Sun set: 18:49
Weather: partly cloudy and light rain
Wind: NE at 15km/hr

Dar es salaam
Temp: 33°C / 25°C
Sun rise: 06:29
Sun set: 18:44
Weather: partly cloudy and sunny periods
Wind: NE at 30km/hr

Mwanza

Temp: 31°C / 19°C
Sun rise: 06:58
Sun set: 19:04
Weather: partly cloudy rain and thunderstorms
Wind: NW at 20km/hr

Dodoma

Temp: 27°C / 19°C
Sun rise: 06:41
Sun set: 19:00
Weather: partly cloudy rain and thunderstorms
Wind: NW at 20km/hr

Tanga

Temp: 34°C / 25°C
Sun rise: 06:32
Sun set: 18:42
Weather: partly cloudy and light rain
Wind: SE at 20km/hr