Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano nchini Tanzania imewapiga marufuku wafanyakazi wake ''Kuchati''
katika mitandao ya kijamii kwa kutumia simu katika muda wa saa za kazi.
Waziri wa Wizara hiyo Makame Mbarawa
amekemea tabia ya baadhi ya wafanyakazi, kutumia muda mwingi maofisini kuperuzi
katika mitandao ya kijamii pamoja na kupiga porojo, hali inayosababisha kushuka
kwa uzalishaji na maendeleo.
Ameongeza kuwa watakaobainika
kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria bila ya kuonewa haya, na pia
kuwataka wafanyakazi wa wizara yake kuwa na bidii ya kazi na weledi.
![]() |
Watu wengi
hutumia simu za mikononi na kompyuta, kwa lengo la kupata taarifa mbalimbali na
pia kujifunza. ( Picha na Maktaba )
|
Lakini hata hivyo, marufuku hiyo
itaweza kufanikiwa?, kutokana na ukubwa wa matumizi ya mtandao, huku walengwa
wakiona wananufaika nayo.
Kutokana na kukua kwa teknolojia ya
habari na mawasiliano duniani, watu wengi hususan vijana wamekuwa wakitumia
muda mwingi katika mitandao ya kijamii, kupitia simu za mikononi na kompyuta,
kwa lengo la kupata taarifa mbalimbali za ulimwengu na pia kujifunza.
Nchini Tanzania matumizi ya huduma
ya mawasiliano imekuwa kwa kasi katika siku za hivi karibuni, hususan kupitia
mitandao ya WhatsApp, Facebook, Twitter na blogi mbalimbali.
Chanzo BBC swahili.
No comments:
Post a Comment