Benki kuu ya Nigeria imesema kuwa
baadhi ya matajiri nchini humo wameficha dola bilioni 20 katika akunti zao za
kubadilishana fedha za kigeni.
Gavana wa Benki Godwin Emefiele
amewaambia mawakili kwamba ufichaji huo unatishia thamani ya sarufu ya
Nigirea,Naira.
Onyo hilo linajiri huku serikali na
benki kuu zikijaribu kudumisha thamani ya sarufi hiyo ambayo kwa sasa
inabadilishana Naira 200 kwa dola moja.
Bwana Emefiele pia amedai kwamba
watu fulani wanaharibu thamani ya Nair kupitia uvumi.
Nigeria hutegemea sana mauzo ya
mafuta ili serikali kupata mapato pamoja na fedha za kigeni.
Kushuka kwa bei ya mafuta
kumepunguza hifadhi ya fedha za kigeni za taifa hilo.
Chanzo BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment