Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa |
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa
ameagiza kutafutwa kwa Ofisa Ardhi wilayani Busega aliyetoa hati na kibali cha
kumuuzia Mtanzania mmoja mwenye asili ya Asia majengo yaliyokuwa yakitumiwa kwa
ujenzi wa barabara ambayo yaligeuzwa shule.
Katika siku ya kwanza ya ziara yake
ya siku sita mkoani Simiyu, Waziri Mkuu ameanza kusaka majipu kwa kuagiza
kusakwa kwa mtumishi huyo wa umma.
Kwa mujibu wa Mbunge wa Busega, Dk
Raphael Chegeni, majengo hayo yaliyokuwa yakitumiwa na kampuni ya ujenzi ya SK
Investment Company Limited, yamebadilishwa hati na kuuzwa kinyemela kwa mtu
aliyemtaja kuwa ni Mtanzania mwenye asili ya Asia.
Dk Chegeni alisema majengo hayo
yalikuwa yakitumika na yanaendelea kutumika kama shule ya sekondari.
Akizungumzia sakata hilo, Waziri
Mkuu Majaliwa aliagiza kusakwa kwa ofisa huyo ili aeleze kwa nini alitoa kibali
na hati hiyo kinyume cha taratibu.
“Wacha hilo la mahakama likamilike,
lakini huyu ofisa ardhi aliyetoa kibali na hati ya kumilikisha aradhi hiyo kwa
Mhindi, asakwe ili aje aeleze nani amempa mamlaka hayo ya kutoa kibali na
hatimiliki,” aliagiza Waziri Mkuu.
Chanzo Habari Leo
No comments:
Post a Comment